Kumbukumbu Uholanzi na visa ya Schengen

Ufanye nini unapokuwa na saa 24 tu za kutalii katika nchi Fulani?hata mimi sifahamu,lakini ngoja nikusimulie kisa changu,pengine utapata cha kufanya. Mwaka 2023,nilipata ufadhili wa masomo ya muda mfupi nchini Uholanzi,ufadhili huo uligharamia safari ya kwenda na kurudi ,malazi na chakula cha asubuhi na mchana,huku tukilipwa yuro kumi kwa ajili ya chakula cha jioni kila siku.Ukweli ni kwamba ilikuwa mara yangu ya kwanza Kwenda bara la Ulaya,nilikuwa na furaha na shauku kubwa sana.Wakati nikijiandaa na safari,nilifanya utafiti na kugundua kuwa,nchi ya Uholanzi ni miongoni mwa nchi mwanachama wa eneo la Schengen,na kwa kupata visa ile nilikuwa na uwezo wa kutembelea takribani nchi 20 zaidi kwa kutumia visa ile moja,nilifurahi sana. Safari ya kutoka Dsm mpaka Amsterdam ilikuwa safari nzuri sana,iliyojaa hamu na ghamu,haswa ikizingatiwa kwamba nilikuwa nasafiri wakati ya ,majira ya Baridi(huko niendako)na nikitoka katika majira ya joto kali nchini mwangu. Kwenye ndege kutoka Ta...